January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuhuma za Kabwili, Simba wainua mikono, waiachia TFF

Ramadhan Kabwili, kipa wa Yanga

Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Simba umetoa taarifa ya kusikitishwa kwao na tuhuma za madai ya rushwa zilizotolewa na mchezaji wa klabu ya Yanga, Ramadhani Kabwili na kufahishwa na hatua iliyochukuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuchunguza swala hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa yao imeeleza kuwa kauli iliyotolewa na mchezaji huyo ina madhala makubwa kwa uadilifu kwa klabu ya Simba na uongozi wake pamoja na TFF.

Baada ya mchezaji huyo kutoa tuhuma hizo kupitia kituo cha East Africa Radio, tarehe 27 Agosti, 2020 tayari TFF imetoa maagizo kwa kamati ya mshindani kuchunguza jambo hilo kwa kuwa ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu.

Katika mahojiano hayo Kabwili alinukuliwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa klabu ya Simba walimpigia simu na kumtaka afanye anachoweza ili apate kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu, iliaweze kuwa na idadi ya kadi tatu za njano na kupelekea kuukosa mchezo unaofuata wa watani wa jadi kwenye msimu uliomalizika 2018/19.

Mchezaji huyo alienda mbali zaidi na kueleza kuwa kama angekubali kufanya hivyo wangempa gari aina ya Toyota IST na huenda wangeibuka na ushindi wa mabao mengi kutokana na kipa aliyekuwepo Claus Kindoki kucheza chini ya kiwango.

Mchezo huo uliochezwa 16 February, 2019 Ulimaliza kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wake Meddie Kagere katika dakika ya 71 huku Ramdhani Kabwili akiwa golini.

error: Content is protected !!