Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tuhuma za CAG: CUF yamtwisha zigo Maalim Seif
Habari za SiasaTangulizi

Tuhuma za CAG: CUF yamtwisha zigo Maalim Seif

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtupia lawama Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wake, kikidai kuwa, alisababisha kikiuke sheria kwa kuhamisha fedha za ruzuku kiasi cha Sh. 300 milioni, kutoka katika akaunti ya chama na kwenda kwenye akaunti ya mtu binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF, jana tarehe 27 Machi 2020 amedai kwamba, chama hicho kilichukua hatua hiyo, kufuatia tishio la aliyekuwa katibu mkuu wake (Maalim Seif), la kuzuia akaunti za chama hizo upande wa Tanzania Bara.

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo, zilizoibuliwa hivi karibuni katika Ripoti ya Ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Naomba nisisitize tukio hili la kuhamisha fedha kwenda akaunti ya Masoud Mhina Omari, lilitokea Januari 2017 kwa sababu ya tishio la kuzuia kutoa fedha toka akaunti za Chama.

Mgogoro wa Chama umemalizika na taratibu za fedha zinazingatia kanuni za fedha za Chama. Tunakubaliana na ushauri wa CAG kuwa “mifumo ya udhibiti wa fedha ndani ya chama uimarishwe kwa kufuata sheria na katiba ya chama.” Hivi sasa Mhasibu anaandaa mfumo imara wa udhibiti wa fedha ndani ya Chama,” amesema Prof. Lipumba.

Katika ufafanuzi huo, Prof. Lipumba amedai kwamba fedha hizo ziliombwa kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa madiwani. Kipindi ambacho CUF kulikuwa na mgogoro, uliosababisha kinyimwe fedha za ruzuku.

“Katika kipindi hiki kulikuwa na tishio la aliyekuwa Katibu Mkuu, kuzuia akaunti zetu zote za Chama upande wa Tanzania Bara zisifanye kazi. Katika hali hiyo Kamati ya Utendaji iliamua Sh 300 milioni, tulizoomba kwa ajili ya kugharamia uchaguzi zihamishwe kwenda kwenye akaunti ya mwanachama muaminifu ili zisije kukwama kwenye akaunti ya chama,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amesema fedha zote zilizowekwa kwenye akaunti ya Omari, zilitumiwa katika masuala ya uchaguzi na uendeshaji wa shughuli za chama. Ambapo wakaguzi wa CAG waliofanya ukaguzi walipewa maelezo  na nyaraka za matumizi ya chama ya mwaka 2016/17.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!