Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tuhuma nzito ziara ya Rais Magufuli
Habari za Siasa

Tuhuma nzito ziara ya Rais Magufuli

Spread the love

ZIARA ya Rais John Magufuli katika gereza kuu la Butimba jijini Mwanza, imeibua tuhuma nzito. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kalikenya Nyamboge, mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka 30 kwenye gereza hilo, mbele ya Rais Magufuli ameibua kwamba, gerezaji hapo ukichomwa sindano, unakufa huku wengine kuporwa mali na maofisa wa gereza hilo.

Hata hivyo, amemweleza rais kuwa, kwa sasa vifo vya wafungwa vimepungua baada ya Jenerali Kamishna (hakumtaja jina) kupeleka mganga msomi mpya.

“Na si mara ya kwanza wao kuua mimi nilikuwa nimepanga nikitoka nije kukwambia na nikitoka nitakuletea mambo yote yanayotokea huku, lakini huyu usimuache maana kwa Mwenyezi Mungu utakua umeandika maelezo ya mauji,” amenukuliwa Nyamboge.

Mfungwa huyo anamthibitishia Rais Magufuli kwamba, kwenye gereza hilo, vitendo vya ajabu vimekuwa vikifanywa na maofisa wa magereza.

Akizungumza madhila gereza hilo, Nyamboge amemtaja ofisa wa usalama wa gereza hilo kuwa kikwazo na mnyanyasaji akidai kuwa, huwapa wafungwa simu kisha wakikutwa nazo baada ya msako huporwa kila kitu.

Akizungumzia wasiwasi wa usalama wake Nyamboge amemwomba Rais Magufuli kuondoka na ofisa huyo kwa kuwa, anaweza kumdhuru endapo atamwacha.

“Mheshimiwa rais, huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo, utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru,” amesema Nyamboge.

Rais Magufuli yupo ziarani Mwanza ambapo leo tarehe 16 Julai 2019, ametembelea gerezani kuu la Butimba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!