October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Tuende na single source’

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kutumia utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ badala ya utaratibu wa kawaida ambao unatumia muda mrefu katika utekeleza wa miradi inayotokana na fedha za zilizotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) nchini. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.

Amesema utaratibu huo wa single source utumike kutafuta wakandarasi pamoja na manunuzi mengine.

‘Utaratibu wetu tenda miezi mitatu hapana…tuende na single source.

“Pia nashauri tathmini ifanyike mapema kubaini vifaa hivyo vya ujenzi na idhini itolewe na  PPRA ili vinunuliwe kwa utaratibu huo niliolekeza” alisema.

error: Content is protected !!