Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TUCTA wampongeza Rais Magufuli, wamkumbusha kilio cha mshahara
Habari Mchanganyiko

TUCTA wampongeza Rais Magufuli, wamkumbusha kilio cha mshahara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Yahaya Msigwa
Spread the love

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limetoa shukrani kwa Rais John Magufuli huku likiambatanisha maombi yake sita ikiwemo kuangalia upya kikokotoo cha mafao kwenye mfuko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika kipindi hiki cha mpito ili kilingane na mifuko iliyokuwa ya LAPF na PSPF. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pia limesema kwa kuwa mshahara wa wafanyakazi bado ni mdogo, hata kikokotoo kikiwa kizuri mafao bado yatakuwa chini, hivyo wanamuomba Rais katika mwaka 2019 ilitazame suala la nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi katika sekta zote.

Maombi hayo yalitolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Umoja wa vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Yahaya Msigwa baada ya maandamano ya amani yaliyofanywa na umoja wa chama hicho kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuweza kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo cha pensheni katika mfuko wa watumishi wa Umma (PSSSF).

Alisema kuwa wanaomba uwakilishi wa wafanyakazi kwenye bodi mbalimbali zilizopo hapa nchini na kwenye bodi za utatu wafanyakazi wawe wengi kwenye uwakilishi.

“Tunakuomba ofisi yako kwa kushirikisha wadau katika kipindi hiki cha mpito kusimamia zoezi la kutengeneza kikokotoo kizuri cha Pensheni.”

Pia alisema kuwa wafanyakazi wanaotumikia taifa hili katika sekta mbalimbali wamejitolea kuwatumikia wenzao katika nafasi wanazozitumikia.

Hivyo wanapomaliza muda wao wa utumishi kazini, wanaporudi makwao warudi kama mashujaa na waajiri wao wawapatie tuzo ya kutambua na kuthamini utumishi wao.

Naye Makamu wa Rais wa TUCTA, Qambos Sulle alisema kuwa wafanyakazi nchini wamefarijika sana na wameguswa kwa jambo alilolifanya Rais.

“Wafanyakazi wengi waliona kama adhabu yaani, lakini kwa usikivu wa Rais wetu ameweza kufanikisha kuiondoa adhabu hiyo hivyo tunamshukuru sana,” alisema.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maandamano hayo ya amani alisema kuwa Serikali ikotayari wakati wote kuyapatia ufumbuzi  matatizo ya wafanyakazi ikiwa ni moja ya njia yakuboresha mishahara na maslahi yao wakati wote wakiwa kwenye utumishi.

“Wito wa serikali kwa wafanyakazi waendelee kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ,weredi na kujituma ikiwa ndio chachu ya kufikia malengo ya ustawi wa maendeleo ya nchi yetu”alisema Majaliwa.

Wakati huo huo alisema kuwa hatua ya uunganishwaji wa mifuko ililenga kuimarisha ,kukidhi kilio chao cha muda mrefu kuhusu kuunganisha mifuko ya pensheni, ili kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko tuliyonayo.

“Hii yote ilikuwa kuondoa ushindani usio na tija baina ya mifuko ya pensheni ambayo kimsingi ilikuwa inatoa mafao yanayofanana, kupunguza migongano baina ya mifuko yanayo huduma kwa watumishi wenye masharti yanayo fanana, muhimu zaidi nikuboresha mafao ya wanachama kwa mifuko ya hifadhi ya jamii,” alisema.

Aidha Majaliwa amewaomba wafanyakazi hao kukubali kushirikiana na mamlaka husika katika kupata muafaka wa jambo hilo kwa siku za usoni kwa kujadiliana kwa njia njema ili kupata kikokotoo sahihi kitakacho tumika baada ya majadiliano hayo.

“Serikali itaendelea kuwashirikisha katika hatua zote zitakazo pitiwa katika kuandaa lakini pia kufanya mnyumbulisho wa kikokotoo hicho ili kufikia hatua ambayo watumishi wote mtaridhika”alisema.

“Viongozi wote wa TUCTA watashirikishwa katika hatua zote, hivyo mchakato utakapoanza tutawajulisha na tutaanza kuleta andiko la kwanza mtalipitia kwa pamoja,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Vijana (U20) kwa Kagera Sugar FC

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!