August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TTCL yacheza ngoma ya Magufuli

Spread the love

 

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema imejipanga kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na kwamba taasisi za umma zinazohamia mkoani Dodoma kutokana na amri ya Rais John Magufuli zisiwe na shaka, anaandika Pendo Omary.

Agizo la kutaka Serikali na Idara zake kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma kabla ya Septemba mwaka huu lilitolewa na Rais Magufuli 23 Julai mwaka huu na kusisitizwa tena  na tena na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim.

Katika taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Nicodemas Mushi, Meneja Uhusiano (TTCL) amesema, “tupo tayari na tuna uwezo mkubwa wa rasilimali watu, vifaa na utaalam wa kutosha katika kutoa huduma za mawasiliano.

“Taasisi zote za umma zinazohamia Dodoma tunazishauri kutumia huduma za TCCL katika kufanikisha malengo yao ya kimawasiliano.”

Hata hivyo, zoezi la kuhamia Dodoma kabla ya Septemba mwaka huu limekosolewa na wanasiasa na wachambuzi wengi wa masuala ya kiuchumi kutokana na serikali kutojipanga vyema ikiwemo kutokuwa na bajeti wala miundombinu inayoweza kuhimili kuhamishiwa kwa serikali na idara zake zote kubwa mkoani humo.

error: Content is protected !!