October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tshishimbi, Molinga, Ngassa watemwa rasmi Yanga

Spread the love

NAHODHA wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi pamoja na mshambuliaji raia wa Congo, David Molinga wameachwa rasmi na uongozi wa klabu hiyo mara baada ya mikataba yao kumalizika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa jumla ya wachezaji waliochwa ni 14 kutokana na mikataba kuisha na wengine kuvunjiwa mikataba yao.

Wachazaji wengine walioachwa baada ya mikataba yao kumalizika ni Mrisho Ngassa, Tariq Seif na Adrew Vicent.

Kwa upande wa wachezaji ambao watasitishiwa mikataba yao ni pamoja na Patric Sibomana, Yikpe, Eric Kabamba, Jafary Mohamed, Mwalami Issa, Ali Ali na Raphael Daud.

Kwa wachezaji watakaoendelea kusalia kikosini hapo ni Farouk Shikalo, Metacha Mnata, Ramadhan Kabwili, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Said Juma, Juma Mahadhi, Feisal Salum, Adeyum Salehe, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama, Benard Morrison na Abdulaziz Makame.

Aidha wachezaji Juma Abdul pamoja na Kelvin Yondan ambao mikataba yao imemelizika wapo katika mazungumzo na uongozi huo kwa ajili ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa mikataba mipya

error: Content is protected !!