Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump: Wauaji Khashoggi walikuwa na mawazo duni
Kimataifa

Trump: Wauaji Khashoggi walikuwa na mawazo duni

Spread the love

SERIKALI ya Saudi Arabia inatokomea kwenye tope baada ya siri za mauaji ya mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post, Jamal Khashoggi kuzidi kumwagika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Utawala wa Mfalme Mohammed Bin Salman umeshindwa kuficha siri iliyopangwa kutunzwa kutokana na mauaji hayo na sasa inakiri kwamba, Khashoggi raia wa Saudia aliuawa kinyama ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini, Instanbul nchini Uturuki.

Hilo halijatosha kutuliza hasira za mataifa ya Magharibi na maneneo mbalimbali ya dunia huku makachero kutoka sehemu mbalimbali wakiendelea ‘kuchimba’ mauaji hayo yanayoonekana kuitikisa Saudia hasa kutokana na taswira yake Ulimwenguni.

Utetezi wa kwamba, Khashoggi aliondoka akiwa salama kwenye ubalozi huo umewekwa pembeni na sasa, Saudia inaeleza kuwa inasaka wale waliotekeleza mauaji hayo kinyume na wajibu wa kazi zao huku ikisisitiza mauaji hayo hayana uhusiano na serikali ya nchi hiyo.

Mshirika wa karibu wa Saudia, Marekani sasa anaishinikiza utawala wa Mfalme Salman kutoka na kuweka mambo hadharani.

Marekani na ulimwengu hawaamini kwamba tukio hilo ni la bahati mbaya kama Saudia walivyotaka kuiaminisha dunia.

Donald Trump, Rais wa Marekani ameilaumu Saudia kwa kile alichokiita ‘harakati za kuzima ukweli’ na kwamba, aliyehusika na mpango huo hatabaki salama.

Marekani wamekuwa katika shinikizo la kuwabana washirika wao Saudia juu ya mkasa huo uliotokea kwenye ofisi zake ndogo za, Instanbul nchini Uturuki.

Akiongea na wanahabari katika Ikulu ya White House, Trump amesema, “Walikuwa na wazo duni sana, na wakalitekeleza vibaya mno, na kiufupi harakati zao za kuuminya ukweli ndio mbovu zaidi katika historia ya kujaribu kuficha ukweli.”

“Naamini aliyekuja na wazo lile yupo katika matatizo makubwa hivi sasa. Na wanatakiwa kuwa kwenye matatizo,” amesisitiza Trump.

Punde tu baada ya kauli ya Trump, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo akatangaza kufutiwa hati za kusafiri za kuingia Marekani kwa watu 21wanaoshukiwa kutekeleza mauaji hayo.

Mamlaka za Saudia zimekuwa zikitoa taarifa za kujikanganya juu ya tukio hilo la kuuwa kwa mwandishi huyo ambaye alikuwa kinara wa kumkosoa Mwanamfalme Mohammad Bin Salman.

Khashoggi, aliingia kwenye ofisi hizo za ubalozi mdogo Oktoba 2 kushughulikia nyaraka za ndoa na hakutoka tena.

Awali Saudia walisema alitoka kisha baada ya presha kubwa ya Uturuki na jumuiya ya kimataifa wakakiri aliuawa alipojaribu kupambana.

Hata hivyo, baada ya maswali kuibuliwa na kutaka uchunguzi ufanyike juu ya huo ugomvi uliosababisha Khashoggi kuuawa, Waziri wa Mambo ya Nje ya Saudia Adel al-Jubeir akakiri kuwa Khashoggi ameuawa katika operesheni isiyo rasmi.

Adel al-Jubeir alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani kwamba “mauaji hayo” yalikuwa ‘makosa makubwa’ na amekana kwamba Mwanamfalme wa Saudia aliagiza mauji hayo.

Jana Jumanne, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa.

Erdogan amesema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki.

Amesema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Ayatollah Khamenei aongoza wairan kumuaga Raisi

Spread the loveKiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Kimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!