DONALD Trump Mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, amesema endapo atachaguliwa kuwa rais hatua ya awali ni kuvunja mikataba ya nyuklia.
Mkataba anaodai kuwa utakuwa wa kwanza kuuvunja ni ule wa Marekani na Iran.
Kwa mujibu wa Trump anaamini mapatano ya mikataba kati ya nchi yake na Iran ni hatari kwa Marekani.
Trump ni mgombea kutoka Republican anayeonekana kuwa na nguvu katika kinyang’anyiro hicho amesema licha ya madhara kwa Marekani pia inaweza kuwa hatari kwa Israel na Mashariki ya kati.
More Stories
Prof. Wajackoyah afanikiwa kupiga kura baada ya kusubirishwa kwa saa tatu
Kenyatta aisifu IEBC: Uchaguzi unaenda vizuri
Trump alia polisi kuzingira, ‘kusachi’ nyumba yake