November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Trump atangaza kugombea urais uchaguzi wa 2024

Spread the love

 

WAKATI kura za uchaguzi wa bunge hazijamalizika kuhesabiwa, rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ametangaza nia ya kugombea urais kwa mara nyingine kupitia chama cha Republikan katika uchaguzi wa 2024.

Hii itakuwa ni mara yake ya tatu kuwania, baada kumshinda mgombea wa Demokrat, Hilary Clinton mwaka 2016, na aliposhindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa 2020. Inaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).

Akiwa katika makazi yake ya Mar-a-Largo, Trump ametoa tangazo hilo huku wachambuzi wakiona ni kama kupuuzia madai ya Warepablikan kwamba ni yeye aliyechangia kukosekana kwa wapiga kura wengi.

Mpaka sasa bado analalamika kwamba uchaguzi uliopita alifanyiwa hila zilizomuwezesha rais wa sasa wa 46, Joe Biden kushinda.

Hata hivyo, anakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa licha ya kwamba kasi yake inaonekana kutozingatia hilo.

Trump ametoa tangazo hilo jana tarehe 15 Novemba, 2022 akiwa na wasaidizi wake kisiasa pamoja na wafuasi wake katika makazi yake ya Mar-a-Largo yaliyopo katika jimbo la kusini la Florida, ambako amekuwa akiishi tangu alipoondoka madarakani mjini Washington, Januari mwaka jana.

error: Content is protected !!