January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Trump ataka pambano na Biden

Spread the love

 

RAIS wa zamani wa Marekani, Donald Trump ameahidi kumpiga Joe Biden ambaye ni Rais wa sasa, kama itatokea likaandaliwa pambano litakalowakutanisha ulingoni kati yao wawili. Anaripoti Glory Massamu TUDARCo … (endelea). 

Trump ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Septemba wakati akizungumzia pambano mabondia Vitor Belfort na Evander Holyfield linalotarajiwa kufanyika kesho huko nchini Marekani.

Katika mpambano huo bondia kutoka Brazili Vitor Belfort (44), atakabiliana na bingwa wa zamani wa Marekani, Evander Holyfield (58).

Aidha, Trump ambaye alikuwa mshereheshaji au ‘MC’ katika hafla hiyo iliyopewa jina la ‘Triller Fight Club Legends 2’, iliyofanyika katika hoteli ya Seminole Hard Rock iliyopo katika jiji la Frlodia.

Akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa mashabiki kwamba ni nani anaweza kukabiliana naye ulingoni, Trump alijibu haraka kuwa ni Biden.

Amesema “Ikiwa ningelazimika kumpiga ngumi mtu, nadhani pengine vita yangu rahisi itakua ya Joe biden, kwa sababu naamini angeenda chini haraka sana.”

error: Content is protected !!