Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump asitisha msaada Palestina
Kimataifa

Trump asitisha msaada Palestina

Donald Trump
Spread the love

DONALD Trump, Rais wa Marekani amesitisha utoaji msaada wa zaidi ya dola 200 milioni kwa Palestina. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Marekani ilipanga kutoa msaada kwa Wapalestina kiasi cha dola 251 milioni, kwa ajili ya kuimarisha utawala bora, afya, elimu na ufadhili wa taasisi za kijamii katika bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2018 ambao unamalizika mwezi Septemba mwaka huu.

Usitishaji huo wa msaada wa Marekani kwa Wapalestina,  umekuja ikiwa imepita miezi kadhaa tangu nchi hiyo kupunguza utoaji misaada kwa Wakala wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA).

Mkurugenzi Mkuu wa Marekani jana Ijumaa tarehe 24 Agosti, 2018 alisema Rais Trump ameamuru idara ya serikali kurekebisha  mipango ya ufadhili kwa Benki ya Magharibi na Ukanda wa Gaza.

Mkurugenzi huyo alisema, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na changamoto zinazokabili jumuiya za kimataifa katika kutoa misaada kwenye eneo la ukanda wa Gaza. Ambapo kikundi cha wanamgambo cha Hamas kimedhibiti maisha ya raia wa gaza na kudhoofisha hali ya kibinadamu na kiuchumi.

Hata hivyo, hatua hiyo ya Marekani imepingwa vikali na Shirika la Uhuru wa Wapalestina (PLO) likidai kuwa imetumika kama silaha ya kisiasa  na kwamba wapalestina na uongozi wao hawatakuwa na hofu na au kupokea mashinikizo yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!