DONALD Trump, Rais wa Marekani amemwagia sifa James Comey, Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi (FBI) akidai ni mtu mahiri na amejipatia umaarufu kiasi cha kumzidi yeye, anaandika Wolfram Mwalongo.
Trump amesema hayo katika tafrija iliyoandaliwa Ikulu ya nchi hiyo iliyohudhuriwa na vigogo wa vyombo vya usalama vya ndani ya taifa hilo.
Hatua hiyo imechukuliwa kama njia ya kurejesha na kumaliza tofauti baina ya rais huyo na shirika hilo ambapo awali lilitoa taarifa za uchunguzi zikishutumu kuwa ushindi wa Trump ulisaidiwa kwa namna mbalimbali na Vladimir Putin, Rais wa Urusi.
Hata hivyo Rais Trump alikana madai hayo kwamba hayana ukweli wowote hivyo yanapaswa kupuuzwa na Wamarekani.
Barrack Obama, rais aliyemaliza muda wake alitilia mkazo na FBI kufanya uchunguzi zaidi na hatimaye taarifa zilithibitisha kwamba Urusi ilihusika katika udukuzi wa kompyuta za Chama cha Democratic ingawa Rais Putini wa Urusi alikanusha madai hayo.
Kwa sasa, mataifa hayo hasimu yanaonekana kupunguza uhasama hasa kutokana na uhusiano mzuri baina ya Putin na Trump.
Leave a comment