October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Trump alikoroga, atuma video ya ubaguzi Twitter

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Spread the love

“NGUVU ya wazungu” ndio maneno ya mfuasi mmoja wa Donald Trump, Rais wa Marekani yaliyomo kwenye video ambayo (Trump) ametuma kwenye ukurasa wake wa twitter. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Mtu anayeonekana kwenye video hiyo ni mfuasi wa Trump aliyeshiriki kwenye kampeni zake Jijini Florida. Kwenye video hiyo, wafuasi wa Trump na wapinzani wa rais huyo wakiwa wakilumbana na kutupiana matusi.

Baada ya kutuma video hiyo, Trump alishutumiwa kwa kusimika mizizi ya ubaguzi katika kupindi hiki ambacho Marekani ilitumbukia kwenye maandamano yasiyokoma kupinga ubaguzi.

Maandamano makubwa yalishuhudiwa nchini humo muda mfupi baada ya polisi wa Minnesota kumuua George Floyd kwa kumkandamiza kwa futi la mguu.

Vitu mbalimbali viliharibiwa huku baadhi ya maeneo yakichomwa moto, kampeni ya kutetea maisha ya watu weusi iliyokwenda kwa jina la ‘Maisha ya Weusi ni Muhimu,’ ilitaala ndani na nje ya taifa hilo.

Mfano; wachezaji wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), siku ya kwanza waliporejea uwanjani baada ya ‘likizo’ ya corona, walifaa jezi zilizoandikwa ‘Maisha ya Weusi ni Muhimu.’

Hata hivyo, Trump amekana kutuma ujumbe huo akiwa na maanda ya kuchochea ubaguzi, amesema wakati akituma video hiyo, hakusikia maneno ya ‘nguvu ya wazungu’ kwenye video hiyo.

Kutokana na malumbano pia shutuma hizo, Trump aliamua kufuta video hiyo kwenye ukurasa wake wa twitter.

Aliwashukuru watu anaoitwa wa vijijini – akimaanisha waliostaafu wanaoishi Kaskazini Magharibi mwa Orlando ambako mkutano huo wa kampeni ulifanyika.

“Wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto hawafanyi lolote, Democrats wataangushwa, Mfisadi Joe Biden (mgombea urais wa Democratic) amepigwa. Tuonane hivi karibuni,” aliandika kwenye ukurasa wake huo.

error: Content is protected !!