Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump ajitosa mgogoro wa Nigeria, Twitter
Kimataifa

Trump ajitosa mgogoro wa Nigeria, Twitter

Donald Trump
Spread the love

 

ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, ameunga mkono hatua ya Serikali ya Nigeria, kuufunga mtandao wa kijamii wa Twitter, nchini humo, huku akitoa wito kwa mataifa mengine kufuata mkondo huo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Tarehe 4 Juni 2021, Serikali ya Nigeria iliifunga Twitter kwa muda usiojulikana, ikijibu hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais wake, Muhammadu Buhari, ulioonya watu wanaochochea matabaka, aliouchapisha tarehe 1 Juni 2021.

Hivi karibuni, Trumpa ambaye pia ni mhanga wa kufungiwa na mtandao wa Twitter, alisema uamuzi huo wa Nigeria, ni mfano wa kuigwa, kwani unatetea uhuru wake kama Taifa lililo huru.

Mapema mwezi Januari 2021, Trump alifungiwa kutumia mtandao wa Twitter pamoja na Facebook, akituhumiwa kuchapisha ujumbe wa kuchochea vurugu katika Bunge la nchi hiyo.

Rais huyo mstaafu wa Marekani, alisema anajuta kwa nini hakuchukua uamuzi wa kufungia mitandao hiyo, alipokuwa madarakani.

Mgogoro wa Serikali ya Nigeria na Twitter, uliibuka baada ya Rais Buhari, kutumia akaunti yake ya mtandao huo, kuwaonya watu waliokuwa wanahamasisha mikoa ya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo, kujitenga.

Katika ujumbe huo, Rais Buhari alikumbushia madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyoibuka nchini Nigeria, kuanzia 1967 hadi 1970.

Ujumbe wa Rais Buhari uliofutwa na Twitter, ulisomeka “wengi waliofanya utovu wa nidhamu leo ni wachanga sana kufahamu uharibifu na upotezaji wa maisha ya watu, uliotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Nigeria. Wale tuliokuwa mashambani kwa miezi 30 ambao tulipitia vita, tutawashughulikia kwa lugha wanayoielewa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!