Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump ajitetea mahakamani kesi ya ngono, alia kuhujumiwa urais
Kimataifa

Trump ajitetea mahakamani kesi ya ngono, alia kuhujumiwa urais

Spread the love

 

RAIS wa zamani Marekani, Donald Trump jana Jumanne amefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kumlipa mwanamke mmoja nyota wa filamu za ngono kabla uchaguzi mkuu wa mwaka 2016, ili asizungumzie uhusiano wa kingono waliokua nao. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Trump amewakosoa waendesha mashtaka nchini humo akisema “wameitusi nchi hiyo.”

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuwasili huko Mar-a-Lago, Florida, baada ya kurudi kutoka New York alikokanusha mashtaka ya jinai dhidi yake.

Trump aliuhutubia umati wa wafadhili, marafiki zake wa kisiasa na wafuasi wake akisema hakudhani kwamba ingetokea mtu kama yeye kufunguliwa mashtaka nchini humo.

Trump amejitetea akisema hajafanya kosa lolote na kwamba mashtaka dhidi yake yanastahili kuondolewa mara moja.

Anadai kuwa kosa lake kubwa lilikuwa kuitetea Marekani kutoka kwa wale wanaonuia kuiharibu.

“Kuanzia mwanzo Wademocrat walikuwa wanachunguza kampeni yangu, mnakumbuka?

Walinishambulia kwa kufanya uchunguzi wa uongo, Urusi, Urusi, Urusi, Ukraine Ukraine, Ukraine, uongo wa kwanza wa kuniondoa madarakani, uongo wa pili wa kuniondoa madarakani, uvamizi wa makazi yangu ya Mar-a-lago hapa,” alisema Trump.

Rais huyo wa zamani ambaye anapigiwa upatu kuipeperusha bendera ya chama cha Republican katika kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2024 amesema waendesha mashtaka kote nchini humo wanatumia kila mbinu ili wampate na hatia.

Amemshambulia mwendesha mashtaka wa Manhattan, Alvin Bragg anayeiongoza kesi hiyo akisema hajui lolote kumhusu na jaji anayeisikiliza hiyo kesi Juan Merchan naye, hakuachwa na Trump kwani amesema jaji huyo ni “jaji anayemchukia Trump.”

Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 76 alikanusha mashtaka 34 dhidi yake katika mahakama ya New York, katika tukio ambalo lilikuwa la kihistoria kwani Trump ndiye rais wa kwanza wa zamani Marekani kufunguliwa mashtaka ya jinai.

Waendesha mashtaka wanasema Trump alidanganya mara kadhaa kuhusu rekodi zake za biashara mjini New York ili kuficha taarifa ambazo zingemchafulia jina kwa wapiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2016 alioushinda.

“Chini ya sheria za jimbo la New York, ni kosa kubwa kudanganya kuhusu rekodi za biashara kwa lengo la kutapeli na kuficha uhalifu mwengine.

“Kesi hii inahusu taarifa 34 za uongo zilizotolewa ili kuficha uhalifu mwengine.

Huu ni uhalifu mkubwa katika jimbo la New York. Hatujali wewe ni nani, unapofanya uhalifu hatuwezi kuuchukulia kama jambo la kawaida,” alisema Bragg.

Wakati hayo yakiendea, Afisa mkuu wa zamani wa masuala ya fedha wa Trump, Allen Weisselberg, kwa sasa anahudumia kifungo cha miezi mitano jela kwa makosa kama hayo ya kutoa rekodi za uongo za biashara.

Trump anatuhumiwa kuwalipa wanawake wawili kabla uchaguzi wa mwaka 2016 ili kuwanyamazisha wasitoe taarifa kuhusiana na mahusiano yao ya kingono.

Wanawake hao wawili walikuwa Stormy Daniels, nyota wa filamu za ngono na mwanamtindo wa zamani Karen McDougal.

Jaji Juan Merchan amesema kesi hiyo itasikilizwa tarehe 4 Desemba 2023, ingawa wanasheria wanadai huenda hata mwaka ukaisha kabla haijasikilizwa.

Wanasheria hao wanasema vile vile kufunguliwa mashtaka au hata kuhukumiwa, kisheria hakutomzuia Trump kugombea kiti cha urais.

1 Comment

  • TBC, TB, TBS, TIB BANK, TBL inawakaribisha wenye mashindano ya mapinduzi (work on talk “mapinduzi”) ya BANGO la Vifo VYA TB, kudhibitisha viwango vya Tabia, uhifadhi wa fedha bank, UJENZI wa BAR nchini Tanzania MTAWALIA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!