Thursday , 29 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Trump agonga mwamba, wahamiaji wapeta 
Kimataifa

Trump agonga mwamba, wahamiaji wapeta 

Spread the love

ZUIO la wahamiaji kuingia nchini Marekani lililotolewa na Donald Trump, rais wa nchi hiyo limefutwa, anaandika Wolfram Mwalongo.

Hatua hiyo imetajwa kuwa kigingi cha kwanza katika utawala wa Trump ambapo rais huyo amevuruga uhusiano wa kidiplomasia na mataifa ya nje.

Ni kutokana na uamuzi wa kutopokea wahamiaji hususani wanaotoka mataifa ya Kiislamu.

Kwa sasa wahamiaji wataendelea kuingia kwenye taifa hilo kutokana na zuio la mahakama mpaka pale kesi hiyo itakapofika tamati.

Aidha, hatua ya kiongozi huyo kufuta visa (vibali vya kuishi) katika taifa hilo kwa raia kutoka mataifa ya Kiislam, imetajwa kama ukikwaji wa haki na kinyume na sheria za nchi hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya Ofisi ya Bob Ferguson’s , Mwanasheria Mkuu nchini Marekani zimesema kwamba, hakuna aliye juu ya sheria hivyo hata akiwa rais anapaswa kufuata sheria.

“Katiba imeshinda leo hii, hakuna aliye juu ya sheria hata akiwa rais,”amesema Ferguson’s.

Rais Trump amesaini sheria hiyo Januari 27 ambapo alisema, lengo ni kuondoa raia wanaotoka mataifa ya Kiislamu ndani ya miezi mitatu.

Alidai kitendo hicho kitaliwezesha taifa lake kubaki salama dhidi ya ugaidi ambapo ncchi hizo ni Iraq, Syria, Sudan, Iran, Somalia, Libya na Yemen.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!