October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TRL washiriki usafi kwa vitendo

Wafanyakazi wakifanya usafi maeneo yao ya kazi

Spread the love

WAKATI Watanzania wakiungana na nchi zingine kuadhimisha siku ya mazingira duniani, Shirika la Reli Tanzania (TRL), wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), wameadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo yao ya kazi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Siku ya mazingira duniani, huadhimishwa June 1-5 kila mwaka, ambapo TRL wameonyesha mfano kwa jamii katika kusafisha mazingira yanayowazunguka.

Akiongoza usafi huo leo jijini Dar es Salaam, katika kituo cha treni kilichopo Posta, Mwenyekiti TRL, Severin Kaombwe amesema, usafi ni muhimu haswa katika mazingira waishio watu ili kuepukana na ajali mbalimbali.

“Kwa kulitambua hilo, ndio maana siku hii tumeitendea kazi, kwa kuwahimiza wafanyakazi wote wa TRL kujumuika kwa pamoja, tusafishe maeneo yetu ya kazi, pamoja na kupanga mikakati ya usafi hata kwenye treni,” amesema Kaombwe.

Aidha, watunishi hao wa TRL pamoja na viongozi wao wamefanya usafi katika maelezo yote ya relini, ikiwemo na kufyeka majani ndani ya kituo hicho.

Naye Mkuu wa Usafirishaji TRL, Lawland Simtenga amesema mbali na kujitaidi kusimamia usafi ndani ya kituo hicho, kwamba bado kuna changamoto zinazowakabili ndani ya treni.

Amebainisha changamoto kubwa wanazokumbana nazo pindi wanapokuwa safarini kuwa ni ubovu wa mabehew kwenye baadhi ya treni, ambapo amedokeza kwamba hutoa moshi mwingi pindi yakiwa safarini, hivyo husababisha uharibifu wa mazingira kwa upande wa hali ya hewa.

Changamoto nyingine ni “hakuna sehemu maalumu ya kuweka uchafu ndani ya treni kwa sasa, tulikuwa tunaweka vitenga vya kuwekea uchafu lakini baadhi ya abiria wanaviba”.

Hata hivyo, Kaombwe katika kutetea madai hayo amesema, “pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo, wizara husika inajua na tupo mbioni kuyatekeleza na kuziondoa changamoto zote ili kuweka mazingira safi”.

Maadhimisho hayo yanabebwa na kauli mbiu ya TRL, “Ndoto bilioni 7 dunia 1, tuitumie rasilimali kwa uangalifu”

error: Content is protected !!