Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Trilioni nane zahudumia deni la Taifa
Habari za Siasa

Trilioni nane zahudumia deni la Taifa

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema hadi kufikia Aprili 2022, imetumia kiasi cha Sh. 8.0 trilioni, kati ya Sh. 10.6 trilioni, ilizopanga kugharamia deni la taifa na huduma nyinginezo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imewasilishwa leo Jumanne, tarehe 7 Juni 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, bungeni jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu amesema, hadi kufikia Aprili, 2022 jumla ya Sh. 29.40 trilioni zimetolewa kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mpango na bajeti ya Serikali, kati ya fedha hizo, Sh. 10.61 trilioni zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati Sh. 7.27 zikitolewa kwa ajili ya kuhudumia deni la Serikali, huku Sh. 6.73 zikitolewa kwa ajili ya mishahara na Sh. 4.79 kwa ajili ya matumizi mengineyo.

“Wizara imeendelea kusimamia deni la Serikali kwa mujibu wa Sheria, wizara imelipa deni lote lililoiva katika kipindi hicho la jumla ya Sh. 6.81 trilioni. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani ni Sh. 4.21 trilioni. Aidha, deni la nje ni Sh. 2.60 trilioni, ikijumuisha riba ya Sh. 0.572 trilioni na mtaji Sh. 2.49 trilioni,” amesema Dk. Mwigulu.

Wakati huo huo, Dk. Mwigulu amesema wizara yake imefanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali kwa miaka 20 ijayo (2021/2022 hadi 2040/41), ambapo matokeo yake yanaonesha kuwa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa pato la Taifa ni asilimia 31.8, ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.

Dk. Mwigulu amesema, hadi Aprili 2022, ukusanyaji wa mapato ya Serikali umefikia Sh. trilioni 19.99, sawa na 93.3% ya makadirio ya kukusanya Sh. trilioni 21.42 , katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yamefikia Sh. trilioni 17.20, sawa na 94.5% ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 18.2.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!