Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tril. 13.3 kugharamia miradi ya maendeleo 2021/22
Habari za Siasa

Tril. 13.3 kugharamia miradi ya maendeleo 2021/22

Ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza
Spread the love

 

TAKRIBANI Sh. 13,326.8 bilioni sawa na Sh. 13.326 trilioni, zinatarajiwa kutumika katika utekelezaji miradi ya maendeleo, kwenye mwaka wa fedha wa 2021/22. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 10 Juni 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa 2020, bungeni jijini Dodoma.

Fedha hizo ni sawa na asilimia 37 ya bajeti ya Sh. 36.26 trilioni, iliyopendekezwa kwa ajili ya matumizi ya 2021/22.

“Kwa mwaka 2021/22, Sh. 13,326.8 bilioni zinakadiriwa kutumika, ili kugharamia miradi ya maendeleo. Kiasi hicho ni sawa na asilimia 37 ya bajeti yote ya Serikali,” amesema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo wa fedha amesema, kati ya fedha hizo, Sh. 6,180.0 bilioni (Sh. 6.1 trilioni), zitatokana na mapato ya ndani, wakati Sh. 4,190.9 bilioni (Sh. 4.1 trilioni) , zitatokana na mikopo ya ndani na nje yenye masharti ya kibiashara.

Huku Sh. 2,955.9 bilioni (Sh. 2.9 trilioni), zitatokana na mikopo nafuu kutoka nje.

“Kati ya kiasi hicho, Sh. 6,180.0 bilioni ni matarajio ya mapato ya ndani, Sh. 4,190.9 bilioni ni mikopo ya ndani na nje, yenye masharti ya kibiashara na Sh. 2,955.9 bilioni, ni misaada na mikopo nafuu kutoka nje,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amesema, fedha hizo zitatumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya kielelezo.

“Sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo, itatumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya kielelezo. Aidha, miradi mingine ya maendeleo, itaendelea kugharamiwa kupitia utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), pamoja na utaratibu wa kampuni maalum (Special Purpose Vehicles),” amesema Dk. Mwigulu.

Ujenzi wa daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam

Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya mpango wa maendeleo wa Taifa wa 2021/22, miradi ya kipaumbele inayotarajiwa kuendelea kutekelezwa katika mwaka huo ni, ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR).

Kwa kujenga kipande cha Morogoro hadi Mkautupora mkoani Dodoma. Pamoja na kipande cha Mwanza hadi Isaka mkoani Tabora.

Miradi mingine ni, wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji. Uboreshaji Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).

Pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa na barabara za juu za Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza), Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!