January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Treni ya umeme yaanza kutumika Ethiopia

Spread the love

NCHI ya Ethiopia imezindua rasmi usafiri za treni ya umeme ya kubeba abiria mijini, ambayo ndiyo ya kwanza katika nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.

Treni hiyo itatumika katika mji mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa kwenye reli ya umbali wa kilomita 34, ikipita mji huo kutoka kaskazini kwenda kusini.

Mradi huo umegharimu $470 milioni (£300 milioni, ukifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Uchina. Mamlaka nchini humo zimesema mradi huo, utafanyakazi kwa saa 16 na unatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani, huku watu milioni moja wakitarajiwa kuutumia kila siku.

Nauli inatarajiwa kuwa chini ya nusu dola kwa kila safari.

error: Content is protected !!