April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TRC yasitisha safari za treni 

Spread the love

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limetangaza kusitisha huduma za usafiri wa treni za abiria na mizigo kwa muda, hasa kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutokana na mafuriko kusomba reli katika maeneo mbalimbali. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa TRC ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Januari 2020, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

“Takriban maeneo 26 yameathirika kati ya hayo 10 yapo katika hali mbaya ambapo tuta la reli na baadhi ya makalavati yamezolewa na maji, tunaomba radhi kwa wadau wa sekta ya miundombinu ya reli iliyoathirika. Matengenezo ya muda yanaendelea katika maeneo ambayo maji yamepungua,” amesema.

Aidha, amesema kuwa utaratibu wa kilipa gharama za abiria waliokwisha lipa nauli unaendelea.

“Mvua hizi zimesababisha nafuriko katika maeneo mbalimbali na kuleta uharibifu mku wa hasa maeneo ya Kilosa (Morogoro), Gulwe (Mpwapwa), Igandu, Zuzu na Makutupola (Singida),” amesema.

Amesema, kusimamishwa kwa usafiri huo kutaendelea mpaka hali itakapo tengemaa na watawajulisha wadau wa sekta ya miundombinu ya ya reli.

error: Content is protected !!