Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TRC waendesha zoezi la kutwaa ardhi kwa ajili ya kupisha ujenzi wa SGR Tabora
Habari Mchanganyiko

TRC waendesha zoezi la kutwaa ardhi kwa ajili ya kupisha ujenzi wa SGR Tabora

Spread the love

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) linaendelea na utekelezaji wa utwaaji ardhi kwa matumizi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) mkoani Tabora katika kipande cha tatu Makutupora –Tabora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRC, timu ya maafisa wa TRC ilianza kwa kufanya uhamasishaji kwa viongozi wa Serikali kwa ngazi ya wilaya, vijiji na kata pamoja na wananchi ambao ni walengwa katika zoezi hilo.

Uhamasishaji umefanyika ukiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi na viongozi kuhusu utaratibu na namna zoezi la kuhamisha makaburi litakavyoendeshwa kwa kuzingatia Sheria ya ardhi na kanuni za afya.

Mara baada ya uhamasishaji zoezi la kuhamisha makaburi lilianza rasmi katika kijiji cha Itulu, kata ya Ndevelwa Manispa ya Tabora ambapo jumla ya makaburi 74 yamehamishiwa katika  sehemu nyingine iliyotengwa na Serikali za vijiji kwa lengo la kupisha ujenzi wa reli ya kisasa.

Katika hatua nyingine, viongozi wa mkoa wametoa wito kwa Serikali ya kijiji na ndugu wa marehemu kutoa ushirikano wa kutosha ili kuhakikisha zoezi linaenda salama na hatimaye kukamilika na mkandarasi kuendelea na ujenzi wa reli ya kisasa ambao hadi sasa umefikia 5.52%

Sambamba na hivyo zoezi limesimamiwa na kuratibiwa na viongozi mbalimbali na wataalamu wa afya, wahandisi, maafisa ardhi, maafisa jamii, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa vijiji, kata, tarafa na viongozi wa Dini.

Hata hivyo zoezi la uhamishaji makaburi ni endelevu kwa sasa limeanza kufanyika katika manispaa ya Tabora katika kijiji cha Itulu na badaye mkoani Singida katika wilaya ya Manyoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!