Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TRA yavunja rekodi, makusanyo yakua kwa 12.2%
Habari MchanganyikoTangulizi

TRA yavunja rekodi, makusanyo yakua kwa 12.2%

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA
Spread the love

 

MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA), imevunja rekodi ya makusanyo ya mapato Kwa mwezi baada ya kukusanya Sh. 2.77 trilioni kati ya lengo la kukusanya Sh. 2.60 trilioni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa Jana tarehe 1 Desemba 2022 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, akitoa taarifa ya makusanyo ya Kodi Kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

“Aidha, TRA inapenda kuutarifu umma kuwa katika kipindi Cha Desemba 2022 imefanikiwa kukusanya kiasi Cha Sh. 2.77 trilioni kati ya lengo la kukusanya Sh. 2.60 trilioni. Makusanyo haya ya Desemba yana ufanisi wa asilimia sawa na ukuaji wa asilimia 10.3 ukilinganisha na makusanyo ya Desemba 2021. Pamoja na makusanyo haya kuvuka lengo la Desemba 2022 ndicho kiwango cha juu zaidi kukusanywa kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa TRA 1996,” imesema taarifa ya Kidata.

Katika hatua nyingine, Kidata amesema makusanyo katika kipindi cha robo mwaka ya kwanza ya 2022/2023, yalikuwa Sh. 12.46 trilioni, ambapo ukuaji wake umeongezeka Kwa asilimia 12.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa 2021/2022, yaliyokusanya Sh. 11.11 trilioni.

“Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 yaani Julai Hadi Desemba 2022, imefanikiwa kukusanya kiasi Cha Sh. 12.46 trilioni ikiwa ni sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya Sh. 12.48 trilioni. Makusanyo haya ni ongezeko la sh. 1.35 ikilinganishwa na kiwango cha makusanyo ya Sh. 11.11 kilichokusanywa kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Ongezeko hili ni sawa na ukuaji wa makusanyo wa asilimia 12.2,” imesema taarifa ya Kidata.

Licha ya ukuaji huo, Kidata amesema ukusanyaji mapato unabidi uongezeke hususan kwa kuinua kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari, ili Serikali ipate mapato ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Aidha, kupitia taarifa yake hiyo Kidata ameishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hasaan, kwa kuiwezesha TRA kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari Mchanganyiko

NBC Dodoma International Marathon kutimua vumbi Julai 23

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetanganza msimu wa nne...

error: Content is protected !!