Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TRA yatangaza neema kwa wananchi
Habari Mchanganyiko

TRA yatangaza neema kwa wananchi

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza fursa ya malipo ya asilimia tatu kwa yeyote atakayetoa taarifa sahihi za kufanikisha kukusanywa kodi iliyokwepa na wafanyabiashara. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Fursa hiyo imetangazwa leo jijini Mwanza jana na Kamishina wa walipa kodi wakubwa wa TRA, Alfred Mregi alipokuwa akizungumza wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya  kodi. 

Akizungumza na wafanyabiashara na wananchi waliohudhuria mafunzo hayo katika eneo la Soko Kuu jijini hapa, Mregi alisema kiwango hicho kinatolewa kama motisha kwa raia wema wanaotoa taarifa za ukwepaji kodi na kufanikisha kodi iliyokwepwa kukusanywa.

“Kila raia mwema anao wajibu wa kulipa kodi na kutoa taarifa za wanaokwepa kodi kwa sababu kodi inayolipwa ndiyo dawa, elimu, miundombinu na miradi yote ya maendeleo na huduma zinazotolewa na Serikali,” alisema Mregi.

Kuanzia juzi Mei 13, 2019, Maofisa wa TRA wanaendesha kampeni ya elimu kwa umma kuwaelimisha wananchi kuhusu kodi ya majengo, kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kodi ya mapato, usajili wa walipa kodi wapya na namna yakulipa kodi ya kielektoniki.

Kwa mjibu wa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TRA, Rachel Mkundai, Mamlaka hiyo pia inatumia fursa hiyo kusikiliza malalamiko, kupokea maoni, changamoto na mapendekezo kutoka kwa walipa kodi.

Akizindua kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Philis Nyimbi aliwahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi bila shurti na kuondokana na usubufu usiokuwa wa lazima.

“Kodi ya majengo inayolipwa kati ya Sh. 10,000 hadi 50,000 ni miongoni mwa maeneo ambayo watu wengi hawalipi kwa wakati na kusababisha msongamano muda wa mwisho unapokaribia,” alisema Dk. Nyimbi.

Dk. Nyimbi pia aliwataka wananchi kudai na kupatiwa stakabadhi kila wanaponunua bidhaa huku akiwaagiza wafanyabiashara wote kuhakikisha wanakuwa na mashine za risiti za kielektroniki (EFDs).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!