August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA yapoteza Bil 1

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepoteza zaidi ya shilingi bilioni moja kutokana na wauzaji wa kanda za muziki na filamu kutobandika stempu halasi za kodi, anaandika Aisha Amran.

Richard Kayombo, Mkurungezi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, MwanaHALISI Online lilikuwepo.

Kayombo amesema, stempu za kodi katika muziki na filamu hutolewa na TRA kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa hizo ili kulinda kazi za wasanii nchini na baada ya hapo ndipo huingizwa sokoni.

“Kwa mujibu wa sheria ya ushuru wa bidhaa kanuni za ushuru wa stempu kwenye bidhaa za filamu na muziki ya mwaka 2012 inasema, watakaobainika watatozwa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu jela,” Kayombo amesema.

Pamoja na hayo TRA imewatahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa kununua bidhaa halali ambazo zimebandikwa stempu za kodi na kuwa, kinyume cha hapo, watoe taarifa katika ofisi yoyote ya TRA.

error: Content is protected !!