January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA yakusanya mil. 258/-za faini

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya kodi na faini ya ya Sh. 258,555, 973 kutokana na bidhaa mbalimbali za magendo zilizokamatwa katika kipindi cha Februari na Machi mwaka huu. Anaandika Sarafina lidwino … (endelea).

Bidhaa hizo zimekamatwa katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera na Arusha katika oparesheni inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya TRA na Jeshi la Polisi kudhibiti uingizwaji wa bidhaa kwa njia ya magendo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo, amesema katika mkoa wa Kagera wamekusanya Sh.120,441,224 kutokana na kukamata katoni 2,043 za pombe aina ya Signature Vodka kutoka Uganda sawa na lita 24,516 yenye thamani ya sh. 61,290,000 zilizokuwa katika jahazi MV Tabasamu TMZ 0541.

Kayombo amesema, kodi ya Sh. 66,736,347 ilipatikana baada ya madumu 1599 ya lita 20 za mafuta ya kupikia yenye thamani ya Sh. 65,990,161 kukamatwa mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa, katika mkoa wa Tanga madumu 888 ya lita 20 za mafuta ya kupikia yenye thamani ya Sh. 15,378,402 yalikamatwa eneo la Kwame katika bandari bubu wilaya ya Mkinga.

“Tunawashukuru sana wasamaria wema ambao wameendelea kutoa taarifa za wanaopitisha bidhaa kwa magendo, na hadi sasa tumekusanya jumla ya lita 2290 za mafuta yenye thamani ya Sh. 2,748,000 yaliyokamatwa Arusha yakisafirishwa kutoka Holili kwenda Moshi kwa magendo,”amesema.

Kayombo ameongeza kuwa mkoani Mwanza pia TRA imekamata lita 50,000 za mafuta ya taa zenye thamani ya Sh.60,000 kutoka Kenya, yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria kwa kutumia jahazi la MV Kalebezo.

Kayombo ametaja maeneo ambayo hutumika sana kuingiza bidhaa za magendo kuwa ni Msasani, Kisiju, Mbweni, Ununio, Mbegani, Bagamoyo, Tanga, Kilwa na Kigamboni.

error: Content is protected !!