July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA yaibuka tena na EFDS

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kupambana na wafanyabiashara wote wasiotumia Mashine za Kutolea Risiti za Kieletroniki (EFDS), anaadika Happyness Lidwino.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Alphayo Kidata, Kaimu Kamishna Mkuu TRA amesema Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 inamtaka mfanyabiashara kununua na kisha kutumia mashine ya kutoa risiti na pia kulipa kodi.

Kidata amesema, pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo, TRA imebaini kwamba, wafanyabiashara waliowengi hawana mashine na wengi walioanza hawazitumii mashine hizo.

“Natoa msisitizo kwa wafanyabiashara wote nchini kutumia mashine hizo, na walipe kodi kwa wakati ili kuipatia serikali mapato. Baada ya serikali kutangaza kutoa mashine hizo bure kwa sasa tunajipanga kutekeleza agizo kwa kuwapatia mashine na wasiolipa kodi tutawachukulia hatua stahiki” amesema Kidata.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imedhamiria kuendesha shughuli za kiforodha kulingana na sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015. Pia Mamlaka itadhibiti ukaguzi na uthaminishaji wa mzigo halisi ili kila mfanya biashara alipe ushuru na kodi kulingana na thamani ya bei husika.

Amesema uthaminishaji mizigo kwa wafanyabiashara umepelekea wengine kulipa kodi kubwa kuliko thamani ya bidhaa husika.

Kidata amesema TRA imefanya uchunguzi hivi karibuni na kubaini kuwepo kwa magari zaidi ya 9,000 yaliyoingizwa nchini na kusajiriwa bila kufuata utaratibu wa forodha na hivyo kufanya yamirikiwe bila kulipa kodi stahiki.

Amesema, pia kumekuwa na matumizi mabaya ya misamaha ya kodi kwa upande wa magari na hivyo kufanya serikali kukosa mapato.

Mbali na hilo Kidata ametoa mwenendo wa makusanyo ya kodi kuanzia Julai 2015 hadi Februari 2016 ambapo kwa mwezi Julai ilikusanya Sh. 8.56 Trilioni ikiringanishwa na lengo la kukusanya Sh. 8.68 Trilioni ambayo ni sawa na asilimia 99.

Kwa mwezi Februari Mamlaka ilikusanya Sh. 10.40 Trilioni kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambayo ni sawa na asilimia 101.18 ya lengo la Sh. 1.02 Trilioni.

Katika mwezi Januari 2016 TRA ilikusanya Sh. 1.07 Trilioni kwa Tanzania Bara na Zanzibar ambayo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la Sh. 1.05 Trilioni. “Makusanyo hayo yote yametokana na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuweka mazingira rafiki kwa walipa kodi.

error: Content is protected !!