MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini matumizi ya namba za magari ambazo hazijatolewa na mamlaka hiyo au taasisi nyingine ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika kaarifa yake kwa umma iliyotolewa tarehe 5, Oktoba, 2022, TRA imeonya matumizi ya namba hizo ambazo huwekwa nyumba na mbele ya magari.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kumekuwepo na matumizi ya vibati vya namba vyenye rangi zisizotambulika kisheria.
“Hivyo wamiliki wa vyombo vya moto na umma kwa ujumla wanatangaziwa kwamba utengenezaji na matumizi ya vibati hivyo ni kosa kisheia kama ilivyoelekezwa kwenye kifungu cha 8 cha Sheria ya Usalama Barabarani,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Huduma na Elimu wa Mlipakodi.
“Hatua kali za kisheria zitachukliwa kwa yeyote anayekiuka Sheria hii ikiwa ni pamoja na kutaifisha chombop cha moto husika.”
Leave a comment