August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA: Wafanyabishara jisalimisheni kila mwaka

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Morogoro imewashauri wateja wake kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kila mwanzoni mwa mwaka, ili kufanyiwa makadirio ya kodi za biashara zao na kuepusha malalamiko hapo baadaye, anaandika Christina Haule.

Morgan Isdori, Ofisa elimu na huduma kwa mlipakodi wa TRA Mkoa wa Morogoro ameyasema hayo alipoongea na wafanyabishara wadogo na wa kati, kwenye warsha ya elimu ya kodi kwa wafanyabishara hao.

Morgan amesema kuwa, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakijisahau kufuatilia makadirio yao na TRA inapowafikishia makadirio hayo, huyaona yapo tofauti na kudai makadirio yameongezwa.

“TRA ni rafiki wa wateja wake. Haiwezi kumuongezea mteja kodi bila ya sababu kwani kufanya hivyo ni kuua mitaji ya wateja na hatimaye kuikosesha makusanyo na mapato TRA,” amesema.

Ameeleza kuwa, makadirio ya kodi ya biashara yanayofanywa na TRA huonekana tofauti, kufuatia mteja biashara nyingine ndani ya biashara aliyokuwa nayo awali, jambo linaloweza kuifanya TRA kuongeza makadirio na kumfanya mteja kuhisi ameonewa.

Hata hivyo, amewaomba wafanyabiashara, kutoa ushirikiano wa kutosha na kuhakikisha TRA inafikia lengo la makusanyo ya Sh. 15.1 Trilion kitaifa kama ilivyopangiwa na serikali.

Evarist Lazaro, mmoja kati ya washiriki wa warsha hiyo, ameiomba TRA kujaribu kuweka utaratibu wa wanunuzi wa pikipiki, kuanza kujisajiri kwanza TRA kisha kununua pikipiki kwani wafanyabiashara hujikuta wakikabiliwa na madeni makubwa ya kodi.

“Mteja hununua pikipiki na kuanza kuitumia kabla hajabadilisha jina toka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi, jambo linasababisha makato ya kodi kwenda kwa muuzaji licha ya kuwa tayari ipo mnunuzi,” amesema.

Helen Mlolele, Ofisa mwandamizi katika ofisi ya huduma kwa mlipakodi TRA Mkoa wa Morogoro, amewashauri wauzaji wa bidhaa hizo kuhakikisha baada ya mauzo wanawapatia risiti bila pikipiki wateja hao na kuwataka kwenda kujisajili upya TRA ili kuepusha usumbufu huo.

error: Content is protected !!