October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TRA: Ukusanyaji kodi umeongezeka kwa 17.4%

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA

Spread the love

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ukusanyaji kodi katika kipindi cha robo ya kwanza ya 2021/2021, umeongezeka kwa asilimia 17.4, ikilinganishwa na ukusanyaji kodi kwenye kipindi kama hicho cha 2020/2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, tarehe 3 Oktoba 2021 na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata.

Taarifa ya Kidata imesema kuwa, katika kipindi hicho, TRA imefanikiwa kukusanya Sh  trilioni 5.151 sawa na ufanisi wa asilimia 94.3, ya lengo la ukusanyaji wa Sh trilioni 5.462

“Makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.4 ukilinganisha na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha uliopita,” imesema taarifa ya Kidata.

Taarifa ya Kidata imetaja sababu za ongezeko hilo, ikiwemo, ukuaji wa ulipaji kodi wa hiari kutoka kwa walipakodi wote hasa kwenye shughuli za uchimbaji madini, mawasiliano na uchukuzi.

Sababu nyingine ni, kuongezeka kwa uwezo wa walipa kodi katika kulipa malimbikizo ya kodi kutokana na Serikali kuongeza kasi ya kulipa marejesho ya kodi.

“Sababu nyingine ni kuimarika kwa mahusiano baina ya TRA na walipa kodi ikiwemo utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama pamoja na kushughulikia malalamiko ya walipakodi kwa wakati,” imesema taarifa ya Kidata.

error: Content is protected !!