August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TRA Morogoro yavunja rekodi ya mapato

Mashine ya kielekroniki (EFD)

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo ya kodi katika kipindi cha robo mwaka kwa kukusanya zaidi ya Sh. 24 bilioni sawa na asilimia 161 tofauti na lengo walilojiwekea na kukusanya Sh. 15 bilioni, anaandika Christina Haule.

Akizungumza na wadau wa kodi wa Manispaa ya Morogoro katika semina ya kodi na matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za (EFD’s) Emmanuel Maro, kaimu meneja wa TRA Morogoro amesema katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka 2016 walitarajia kukusanya Sh. 15.3 bilioni lakini wamepata Sh. 24.6 bilioni.

“Makusanyo haya yametokana na kodi za ndani na kodi za forodha, tumefanikiwa kukusanya fedha hizo baada ya walipakodi kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kufuatia matangazo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na TRA kwa kutumia magari ya matangazo na kampeni ya matumizi ya mashine za EFD’s,” amesema Maro.

Hata hivyo amedokeza kuwa TRA inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo namna ya kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma katika wilaya za Malinyi na tarafa ya Mlimba huku mifumo ya matumizi ya ndani katika vituo vya Kilombero, Kilosa, Mvomero, Ulanga na Gairo ikikosekana jambo linaloleta shida katika ukusanyaji wa kodi na uhifadhi wa kumbukumbu.

“Pamoja na hayo, walipakodi hakikisheni mnalipa kodi kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopo, waepukeni ‘vishoka’ kwa kuingia wenyewe kwenye ofisi husika na kupata huduma ili kuwakwepa wanaojifanya ni maofisa wa TRA ilihali ni matapeli,” amesema.

error: Content is protected !!