Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA kutumia uwajibikaji, uadilifu kutimiza malengo 2021/22
Habari Mchanganyiko

TRA kutumia uwajibikaji, uadilifu kutimiza malengo 2021/22

Spread the love

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ili kuhahakikisha inafikia lengo la kukusanya zaidi ya Sh.22.18 trilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022 watazingatia, weledi, uwajibikaji na uadilifu. Anaripoti Seleman Msuya, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa na Ofisa Msimamizi wa Kodi TRA, Joyce Ng’oja wakati akiwasilisha mada jana Ijumaa tarehe 3 Septemba 2021, kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha 2021 kwa waandishi wa habari wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC).

Ng’oja alisema, Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango wamekuwa wakifanya maboresho na marekebisho ya mbalimbali ambayo yawezesha TRA kukusanya kodi kwa ufanisi.

Alisema kutokana maboresho hayo TRA imekuwa ikiongeza wigo wa ukusanyajii kodi jambo ambalo litawezeshalengo lao la kukusanya Sh. trilioni 22.18 kufikiwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

“TRA imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa makundi yote ambayo yanahusika katika ulipaji kodi na watoa elimu kama nyie waandishi, lakini pia katika mchakato mzima lazima tuzingatie weledi, uwajibikaji na uadilifu,” alisema huku akisema

Ofisa huyo alitoa msisitizo kwa waandishi wa habari kusoma sheria mbalimbali ambazo zinahusu masuala ya kodi ili kuhakikisha wanatoa elimu sahihi kwa jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, alisema mamlaka hiyo imedhamiria kuwatumikia Watanzania kwa kukusanya kodi kwa haki ili kusaidia serikali kufanya shughuli za kimaendeleo.

Alisema, TRA pia inafanya kazi zake kwa kusimamia misingi ya mpango mkakati katika uwajibikaji uadilifu na weledi pamoja na kutoa elimu kwa walipa kodi kujua haki zao kama walipa kodi.

Sambamba na hayo alisema kutokana na changamoto inayoikumba Dunia kwa sasa ya Covid 19 TRA imebadili mufumo wa utoaji huduma kwa baadhi ya huduma ambapo mteja anaehitaji TIN ataipata kwa njia ya kielektroniki.

Hata hivyo alisema huduma ya mnada pia imehamia katika njia ya kielektroniki ili kuongeza ufanisi na ushindani wa haki kwa washiriki ambapo kwa sasa utajumuisha nchi nzima tofauti na awali kufanyika Dar es Salaam peke yake.

Alisema pia katika utendaji wao wa kazi wanawashirikisha wananchi ambapo kila mwezi Desemba Wizara ya Fedha hutoa tangazo kwa wananchi la kutoa maoni na kuuliza maswali ambayo Waziri wa Fedha huyatumia kwenye mapendekezo yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DCPC, Irene Mark ameishukuru TRA kwa mchango wao wa hali na mali kwa klabu hiyo huku akiwatak waandishi kutumia kalamu zao kutoa elimu kuhusu dhana nzima ya ulipaji kodi.

Aidha, Mark aliwashauri waandishi wa habari nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya kuchanja chanjo ya Uviko-19 ambayo inatolewa nchini.

“Sisi ni watu ambao tunasikilizwa na watu wa makundi mengi, naomba tutumie tasnia yetu kuandika habari za kodi ili jamii iweze kuelimika. Pia tujitokeze kuchanja Uviko-19 ili tuweze kuwa salama,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!