Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA kuchunguza kipato cha Askofu Kakobe
Habari Mchanganyiko

TRA kuchunguza kipato cha Askofu Kakobe

Askofu Zacharia Kakobe, picha ndogo Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere
Spread the love

BAADA  ya kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Askofu Zacharia Kakobe kudai ana fedha nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kuanza kufuatilia ulipaji wake wa kodi. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema mamlaka yake imeipokea kwa furaha kauli ya Askofu Kakobe na inataka kujiridhisha vyanzo vya utajiri huo.

Kichere amesema TRA inafahamu kuwa shughuli za kidini hazitozwi kodi lakini inataka kufahamu kama fedha hizo za Askofu Kakobe zinatokana na sadaka pekee au kuna shughuli nyingine za kiuchumi.

“Tumefuatilia hakuna kumbukumbu za Askofu Kakobe kulipa kodi, sasa tumeona tumfuate maofisa wetu wakajiridhishe kama fedha hizo anazozizungumzia zinatokana na sadaka,” amesema Kichere na kuongeza:

“Na kama hana shughuli zozote za kiuchumi ikiwa ina maana utajiri huo unatokana na sadaka ni jambo la kushtua kidogo lakini sisi tutaishia hapo.”

Amesema katika taarifa za mamlaka hiyo wapo watu wengi wenye fedha nyingi na kumbukumbu zao za kodi zipo lakini Askofu Kakobe si miongoni mwao.

Kichere amemwomba Askofu Kakobe kutoa ushirikiano kwa maofisa wa TRA watakaomtembelea kwa ajili ya shughuli hiyo ya ukaguzi.

Kuhusu kwanini uhakiki huo umekuja sasa Kichere amesema ni baada ya kusikia ana fedha nyingi kuliko Serikali wakati anafahamika ni kiongozi wa taasisi ya dini.

TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI KUJUA ALICHOSEMA ASKOFU KAKOBE MWANZO MWISHO…Usisahau kusubcribe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!