Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Biashara TPHPA yafunda wafanyabiasha, wakulima matumizi ya viuatilifu
Biashara

TPHPA yafunda wafanyabiasha, wakulima matumizi ya viuatilifu

Spread the love

MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imetoa mafunzo kwa wakulima ili waweze kutumia viuatilifu vilivyosajiliwa kwa usahihi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mratibu wa Mafunzo kutoka TPHPA, Jumanne Rajabu Jumanne, huku akibainisha kuwa wafanyabiashara, watafaidika kuweza kusambaza viuatilifu sahihi na kutoa taarifa na maelekezo sahihi ya namna ya kutumia viuatilifu.

Amesema katika mafunzo hayo ya huduma wima kuhusu matumizi sahihi na salama ya viautilifu yataweza kusaidia wakulima na wafanyabiashara na sekta ya kilimo itakuwa.

Rajabu amesema mafunzo yanayotolewa na mamlaka hiyo kwa wakulima, yatawawezesha kutumia viuatilifu kwa usahihi na kutambua viuatilifu vilivyosajiliwa Tanzania na Mamlaka ya TPHPA kwa sababu viuatilifu vilivyosajiliwa ndivyo vilivyohakikiwa kisayansi kukidhi matakwa ya usalama wa afya ya binadamu, wanyama au mazingira na ufanisi katika kudhibiti visumbufu.

“Katika kutumia viuatilifu, kupitia mafunzo wakulima wanaweza kujua kanuni bora za unyunyiziaji na upuliziaji wa viuatilifu ikiwa ni pamoja na uchaguzi sahihi wa vifaa vya kunyinyizia,” amesema.

Amesema idadi kubwa ya wakulima wanawategemea wafanyabiashara kupata maelekezo ya kutumia viuatilifu, hivyo mafunzo hayo yataongeza wigo mpana.

Rajabu amesema maafisa kilimo; wataongeza ujuzi wa kutambua shabaha kwenye maeneo mahususi ya mimea, ili kutoa maelekezo sahihi ya kudhibiti visumbufu kwa kutumia viuatilifu na mbadala sahihi kwa ajili ya ufanisi katika kudhibiti visumbufu ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo

“Watumiaji wote wa viuatilifu wataweza kujikinga kwa kutumia vifaa sahihi vya kuzuia viuatilifu kuingia mwilini kwa kuwa viuatilifu ni kemikeli zenye madhara kiafya,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

Biashara

Kasino ya Lucky Sevens ni rahisi kucheza na kuibuka tajiri, fanya haya

Spread the love  NENO Kasino unapolisikia kwa mara ya kwanza unapata picha...

Biashara

Ujenzi waiva barabara ya Bigwa – Kisaki

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa mkandarasi atakayetekeleza ujenzi...

Biashara

Fanya haya kabla hujacheza kasino

Spread the love  UNAPOANZA kufikiria jinsi ya kutengeneza pesa kirahisi usipate shida,...

error: Content is protected !!