August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TPDC yatengewa Bil 1.5

Spread the love
JUMLA ya Sh 1.5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya   maendeleo ya Shirika  la Maendeleo ya Petrori Tanzania(TPDC) kwa mwaka wa fedha 2016/17, anaandika Aisha Amran.
Kati ya fedha hizo, fedha za ndani  ni Sh 700 mil ni kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa kusambaza gesi asilia kwa Mkoa wa Mtwara na Lindi na Sh. 800 mil kwa ajili ya mradi wa kuchakata gesi asilia na kusafirisha nje na ndani ya nchi na Sh. 9.2 bil fedha za nje.
John Mnyika, Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Nishati na Madini ameyasema hayo wakati akitoa maoni kuhusu Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2015/16 na makadilio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Amesema licha ya kutengewa fedha hizo kwa mwaka wa fedha 2016/17, lakini shirika kwa mwaka wa fedha 2015/16 liliomba kiasi cha shilingi 12bilioni kama fedha za maendeleo cha kusangaza hadi kamati za Bunge zinakutana kwa mwaka wa fedha mpya hakuna hata shilingi iliyokuwa imetolewa na hazina kama fedha za maendeleo.
“katika biashara yoyote kuonesha hali ya unyonge maana yake ni kuweka haki rehani na ndivyo TPDC kukosa fedha za miradi ya maendeleo ni kuweka sekta ya mafuta rehan”i.
“ukosefu wa fedha unaolikumba shirika hilo ndio unapelekea mapato ya gesi kutokukusanywa kwa kadri mikataba na sheria zinavyosema” .
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya TPDC inaonesha kuwa Songas inadaiwa jumla ya shilingi 50,275,344,006 na Pan African Energy inadaiwa jumla ya shilingi 60,665839,011 kwa hali gesi haitaweza kuwa na manufaa kwa wananchi kutokana na kuwa na madeni yanayoshindwa kudaiwa kwa kusimamia mikataba iliyopo.
Mnyika amesema sambamba na hilo pia shirika hilo limeshindwa kupokea gawio kutoka kwa Songas lenye thamani ya dola za kimarekani 467,997 na kuzidi kuwa hoi kifedha.
“tunaitaka serikali itoe majibu ya haraka katika bajeti za nyuma kwanza na muundo mpya wa utendaji wa TPDC ambao ulikua unatia mashaka japokuwa ulipata Baraka zote za wizara ya nishati ya madini”.amesema Mnyika.
error: Content is protected !!