Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TPA yapewa wiki 2 bandari ya Karema ianze kutoa huduma
Habari Mchanganyiko

TPA yapewa wiki 2 bandari ya Karema ianze kutoa huduma

Spread the love

NAIBU Waziri Uchukuzi, Atupele Mwakibete ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha bandari mpya ya Karema inaanza kutoa huduma ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kwa mikoa inayozunguka Ziwa Tanganyika na nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo mkoani humo ambao umekamilika kwa asilimia 100, Naibu Waziri Mwakibete amesema kukamilika na kutoa huduma kwa bandari hiyo iliyogharimiwa na Serikali kwa fedha za ndani zaidi ya shilingi bilioni 30 kutachochea uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

Kaimu Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika Edward Mabula akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete baadhi ya miundombinu ya bandari iliyokamilika, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Karema Mkoani Katavi.

“Fedha nyingi zilizowekwa hapa lazima zianze kutumika vitu vilivyobaki ni vichache sana na viko ndani ya uwezo wetu hivyo tuvikamilishe haraka na tuanze kutoa huduma muda hausubiri na mradi umeshakamilika”, amesisitiza Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete amesema pamoja na mradi huo Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 inaendelea na ukarabati wa meli ya MT. Sangara na imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya mbili za abiria na mizigo zitakazotoa huduma katika Bandari za Ziwa Tanganyika na nchi za jirani.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewataka TPA kuhakikisha wananchi wa Kata ya Karema wanapewa kipaumbele cha ajira hususani kwa kazi zisizohitaji utaalam sababu ajira hizo zitachochea uchumi wao pia walinzi wa miundombinu hiyo ili iweze kudumu.

Muonekano Mzani uliopo ndani ya Bandari ya Karema Mkoani Katavi. Mzani huo ni sehemu ya miundombinu iliyojengwa kwenye mradi wa Ujenzi wa Bandari hiyo ambayo kwa sasa umekamilika kwa asilimia mia moja na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 30.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu .ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuunda vikundi vidogo vidogo  ili kutumia fursa ya uwepo wa mradi huo mkubwa kupata ajira za muda mfupi na mrefu wakati itakapoanza kufanya kazi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula, amesema mradi kwa sasa umeshakamilika na kumuhakikisha Naibu Waziri kuwa kazi zilizobaki ni kufunga umeme kazi itakayofanyika kwa wiki moja  pamoja na uletaji wa mitambo ya kuhudumia mizigo.

“Mhe. Naibu Waziri huduma hapa itaanza wakati wowote sababu baada ya kuunganisha umeme, tutafanya majaribio kwa siku chache na baadae tutakamilisha taratibu za uendeshaji na tutaanza kutoa huduma” amesema Kaimu Meneja   Edward Mabula.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mwakibete yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya siku  mbili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!