June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TPA yahimizwa kutumia Elektroniki

Spread the love

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imewata mawakala wa ushuru na forodha katika bandari ya Dar es Salaam, kutumia mfumo wa malipo wa kielektroniki wanayofanya na wateja wao, watumiaji wa bandari hiyo ili kurahisha huduma zitolewazo na bandari hiyo pamoja na kuondoa msongamano wa mizigo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa na Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Focus Mauki alipokuwa akaizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Maelezo Jijini Dar es Salaam.

Mauki amesema kuwa mfumo huo utamuwezesha mteja kupata mzigo wake kwa kufanya malipo katika benki mbalimbali kupitia mfumo huo wa kieletroniki

Amesema kuwa kupitia mfumo huo mteja ataweza kuona na kulipia kiasi cha ushuru alichokuwa anadaiwa na kuhakiki mzigo kabla hayaulipia ili kuepusha upotevu wa mizigo

Mauki amesema kuwa mfumo huo utamwezesha mteja kujua gharama za kulipia mzigo na kulinganisha gharama ambazo angelipia mzigo huo kupitia wakala.

“kupitia benki mbalimbali, mitandao ya simu za mikono kama vile Airtel Money, Tigo Pesa na M-pesa, mteja anaweza kulipia ushuru na malipo forodha na kumrahisishia wakala wanao tuma mizigo hiyo kwa wateja kutokuja kwenye ofisi zetu”amesema Mauka

error: Content is protected !!