
Magari yakiwa katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam yakisubiri kuchukuliwa na wahusika
MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imechangia jumla ya Sh. Milioni 209.87 kwa ajili ya huduma za jamii na majanga kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi (CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua, ni mapato kiasi gani yamepatikana katika Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka mitatu kuanzia 2012 kurudi nyuma.
Pia, alihoji Jiji la Dar es Salaam au halmashauri zake zimepata gawio kiasi gani la mapato hayo kwa miaka hiyo.
Aidha, alitaka kujua TPA imechangoa kwenye huduma gani za jamii katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akijibu swali hilo Tizeba amesema, kwa miaka mitatu iliyopita TPA ilichangia Sh. Milioni 209.87 kwa ajili ya huduma ya jamii na majanga.
Amesema, fedha hizo zilitumika katika sekta za afya, elimu na moja kwa moja kusaidia waathirika wa majanga kama vile mafuriko na kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Amesema, Jiji la Dar es Salaam au halmashauri zake hazipati gawio la mapato ya Bandari kwa kuwa si wanahisa.
More Stories
Wanaharakati ‘wawaangukia mawakili wanawake
Wanakijiji DRC wavamia mlima wa dhahabu
Mgomo wa mabasi wanukia Tanzania