Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Tozo miamala ya simu yapingwa mahakamani
Tangulizi

Tozo miamala ya simu yapingwa mahakamani

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC), kimefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga tozo za miamala ya simu, zilizoanza kutumika tarehe 15 Julai 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga.

Katika kesi hiyo, LHRC inapinga tozo hiyo kwa madai kwamba ni mzigo kwa wananchi, hasa wasio na uwezo wa kifedha.

“LHRC kimefungua kesi hiyo kufuatia kupitishwa kwa mapendekezo ya Bajeti ya Serikali 2021/22, pamoja na sheria ya fedha iliyopelekea kuweka tozo katika miamala ya fedha, inayofanywa kwa njia ya simu. Jambo ambalo limeongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida, pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakubwa,” amesema Henga.

Mkurugenzi huyo wa LHRC amesema, wanaiomba mahakama hiyo ipitie Sheria ya Mfumo wa Malipo ya Kitaifa Sura. 437, pamoja na kanuni zake zilizoweka tozo hiyo, ili iamuru Serikali kuiondoa au kupunguza viwango vinavyotozwa kupitia tozo hiyo.

“Katika kesi hii tunaomba viwango vipunguzwe kama itakuwa lazima iwepo au iondolewe. Kwa sababu tunaona mzigo zaidi kwa wananchi ambao wanalipa kodi na wanapokuwa wanatoa pesa wanakatwa kodi na tozo kwa kiasi fulani,” amesema Henga.

Henga amesema kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 27 Julai 2021 na ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, tarehe 5 Agosti 2021 mbele ya Jaji John Mgeta.

“LHRC kilifungua shauri la namba 11 ya mwaka 2021, kuomba mapitio ya Mahakama Kuu (Judicial Review), kuhusu National Payments System Act Cap. 437, pamoja na kanuni zake zilizoweka tozo katika miamala ya fedha kwa njia ya simu,” amesema Henga.

Henga amesema, kesi hiyo itasikilizwa tena mahakamani hapo kwa mara ya pili, tarehe 16 Agosti 2021.

Tangu tozo hiyo ianze kutumika, makundi mbalimbali yaliipinga kwa maelezo kwamba ni mzigo kwa wananchi na kuiomba Serikali iiondoe au ipunguze viwango vyake.

Tarehe 27 Julai 2021, akiwaapisha mabalozi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan, alisema Serikali yake inayafanyia kazi malalamiko hayo kuhusu tozo hiyo.

Rais Samia alisema Serikali yake haitaiondoa tozo hiyo, bali itaangalia namna bora itakayowezesha wananchi kuilipa bila maumivu.

2 Comments

  • Tozo zingine ni zile za benki ambazo ni kero kubwa. Kwa mfano benki ya NMB ukichukua fedha zako unatozwa pamoja na kodi ya serikali. Kadi ya kitambulisho nacho kinatozwa kila mwezi pamoja na kodi. Ukiuliza salio au statement halikadhalika tozo kodi tozo kodi. Duniani kote benki hazitozi tozo kama hapa kwetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!