Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Tozo miamala ya simu yajenga Kituo cha afya Musoma
Afya

Tozo miamala ya simu yajenga Kituo cha afya Musoma

Spread the love

JUMLA ya Sh milioni 250 zilizopatikana kutokana na tozo za miamala ya simu zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya Rukuba kilichopo Musoma vijijini mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (CCM) alipotembelea ujenzi wa kituo hicho jana tarehe 4 Machi, 2022.

Aidha, baadhi ya wakazi wa Rukuba wameelezea furaha yao kutokana na ujenzi wa Kituo hicho na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii nchini.

Pamoja na mambo mengine Kituo hicho cha afya, kitakuwa na maabara ambayo jengo lake limekamilika, wodi ya mama na watoto ambayo ujenzi wake upo ngazi ya msingi na jengo la kituo kizima ambalo lipo ngazi ya kukaribia kuezekwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!