WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania imesema, tozo ya asilimia sita inayotozwa kila mwaka na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), itaondolewa rasmi kuanzia tarehe 1 Julai 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako leo Jumanne, 4 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2021/22.
Ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa Mei Mosi 2021, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi dunia ambapo alisema, tozo hiyo ya asilimia sita inaifuta na itabaki ile ya asilimia 15 inayokatwa kwenye mshahara kila mwezi.
Akiwasilisha bajeti yake, Profesa Ndalichako amesema, Serikali itaondoa tozo ya asilimia sita ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji wa mkopo kuanzia tarehe 1 Julai, 2021 iliyokuwa inatozwa kwa wanufaika.
“Aidha, Serikali inaiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuondoa pia tozo ya adhabu ya asilimia 10 ya mkopo ambayo inatozwa kwa wanufaika wanaochelewa kulipa mikopo hiyo,” amesema
Leave a comment