January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Toa chakula tujenge maabara’

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete

Spread the love

VIONGOZI wa halmashauri nchini wanahaha kukamilisha utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kujenga maabara tatu katika shule za sekondari za kata.

Lakini Halmashauri ya Jiji la Mwanza imefuja Sh. Bilioni 40.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa ambaye amehamishiwa Mkoa wa Dodoma katika mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa wiki iliyopita, amefuta safari za viongozi wa kisiasa – madiwani – pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, mpaka wakamilishe maabara zilizopangwa.

Agizo la Rais Kikwete ambalo lilitolewa Novemba mwaka uliopita, linatekelezwa kwa kutumia mgambo ambao wanalazimisha wananchi wachangie gharama za ujenzi wa maabara hizo.

Viongozi wa Halmashauri wameamrisha msako wa watu kwa lengo la kuwalazimisha kutoa fedha na kama hawana fedha taslim, watoe mifugo au chakula chenye thamani ya fedha zilizotajwa.

Lakini ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambayo ina tatizo la kutopata madawati ya kutosha kwa ajili ya shule za serikali, inatoa msaada wa Sh. 100 kutengeneza madawati.

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imethibitishwa kutumia vibaya Sh. 20 bilioni zikiwemo Sh. 9 bilioni za kugharamia mkutano wa siku moja wa menejimenti na wafanyakazi wa mamlaka.

Hayo yanagundulika wakati tayari Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – Controller and Auditor General (CAG) – amebaini ufisadi wa Dola 124 milioni uliohusisha fedha za TANESCO/IPTL ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika akaunti maalum ya Escrow, iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ufisadi katika serikali ya CCM umeshika kasi huku athari zake zikiangukia wananchi ambao hawana cha kufanya.

error: Content is protected !!