June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TMF yatimiza miaka minane

Spread the love

MFUKO wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) inatarajiwa kuadhimisha miaka minane ya mafanikio katika kuongeza uwajibikaji kwa kuimarisha sekta ya habari nchini yatakayofanyika Septemba 22, 2015. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Mkurugenzi wa Mfuko huo, Ernest Sungura amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaama kwamba maadhimisho hayo yatajumuisha maonyesho ya kazi za waandishi wa habari waliowezeshwa kwa misaada na mfuko huo kwa lengo la kuongeza uwajibikaji serikalini.

Sungura amesema kutakuwa na utoaji wa tuzo katika maadhimisho hayo kwa waandishi walioleta mabadiliko chanya kwa jamii kutokana na msaada wa TMF.

Pia amesema maadhimisho hayo yatatoa fursa ya mijadala itakayochangiwa na wanaharakati mbalimbali kutoka asasi za kiraia.

“Tangu mwaka 2008 mfuko umetoa misaada kwa waandishi wa habari zaidi ya 570 kutoka vyombo zaidi ya 120 nchi nzima ,” amesema Sungura.

Misaada iliyotolewa na mfuko huo imelenga katika kuongeza uwezo wa waandishi wa habari katika kuandika habari za uchunguzi kwenye maeneo mbalimbali kama vile uchimbaji, matumizi ya fedha za halmashauri katika sekta za afya, elimu, miradi ya maji na miundombinu.

error: Content is protected !!