MFUKO wa Vyombo vya Habari nchini (TMF) umesisitiza azma yake ya kuendelea kusaidia waandishi wa habari katika kuwaongezea umahiri ili kuimarisha sekta ya habari nchini, anaandika Faki Sosi.
Katika semina fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ikishirikisha TMF na waandishi wa habari imeelezwa kuwa, taasisi hiyo imejipanga kuendeleza ufadhili kwa waandishi wa habari ili kuandika habari za kiuchunguzi na zenye maslahi kwa jamii.
Dastani Kamanzi, Ofisa wa TMF amewahimiza waandishi kujitokeza na kuomba ruzuku ili kwenda kuandika habari ambazo zitakuwa na matokeo chanya kwa jamii pia kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Kamanzi amesema kuwa, kuna waandishi walinufaika kupitia TMF na wapo waliokosa uaminifu kwa kutofanya kazi aliyotakiwa kufanywa.
More Stories
DUWASA wakata maji Soko la Mavunde, wafanyabiashara walia
Mkurugenzi Mkuu UNESCO Duniani atoa ujumbe siku ya Kiswahili duniani
Simbachawene kuongoza harambee kampeni GGM Kili Challenge 2022