April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TMA yatoa utabiri wa hali mbaya ya hewa

Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa, kwa siku tano kuanzia jana Jumanne tarehe 5 hadi 9 Mei 2020, katika mikoa zaidi ya mitano ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA, jana Jumanne kulikuwa na angalizo la kutokea kwa mvua kubwa maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Pwani pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.

“Athari zinazoweza kujitokeza, baadhi ya makazi kupata mafuriko pamoja na baadhi ya barabara kutopitika, kuathirika kwa baadhi ya shughuli za usafirishaji,” inaeleza taarifa ya TMA.

Jumatano ya leo tarehe 6 hadi 9 Mei 2020, TMA imetoa tahadhari ya kutokea upepo mkali kwenye baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kusini na Kaskazini, Ukanda wa Ziwa Nyasa na Kusini mwa Ziwa Tanganyika.

“Angalizo la upepo mkali limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini, Kusini na ya Bahari ya Hindi. Ukanda wa Ziwa Nyasa pamoja na kusini mwa ziwa Tanganyika, Uwezekano wa kutokea ni mkubwa na kiwango cha athari zake ni cha wastani,” inaeleza taarifa ya TMA.

Mamlaka hiyo imesema uwezekano wa kutokea hali hiyo ni kubwa na wa wastani katika baadhi ya maeneo huku athari zinazoweza kujitokeza zikitajwa ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafiri baharini.

“Uwekano wa kutokea upepo mkali ni mkubwa na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni cha wastani. Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafiri baharini, ugumu wa upatikanaji wa samaki,” inaeleza taarifa ya TMA.

error: Content is protected !!