December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TMA yatangaza mvua kubwa Dar

Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kunyesha mvua kubwa kesho Jumanne tarehe 24 Novemba 2020 baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 23 Novemba 2020 na TMA imesema, kuna uwezekano wa kutokea wastani wa kiwango cha athari kutokana na mvua hizo.

TMA imesema, baadhi ya makazi huenda yakazungukwa na maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

error: Content is protected !!