Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa
Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kutangaza mafanikio ya taasisi yanayopatikana kikanda, kimataifa pamoja na mafanikio yanayopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Prof. Kahyararaameta maagizo hayo alipotembelea banda la maonesho la TMA katika Mkutano wa 16 wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini (16th JTSR) unaofanyika jijini Arusha, leo tarehe 5 Desemba 2023 ambapo pia ameisifu TMA kuwa ni taasisi inayofanya kazi nzuri na yenye mafanikio kitaifa na kimataifa.

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa; “Ni wakati sasa, jamii ikatambua mafanikio ya TMA kikanda na kimataifa, natambua kuwa taasisi hii inafanya kazi nzuri inayoonekana, ni vyema kujipanga kuwa na vipindi katika televisheni na kueleza mafanikio hayo.”

Aidha, Katibu Mkuu aliitaka Wizara kusimamia program ya kutangaza mafanikio ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa kuanza na TMA.

Naye, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TMA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Miundombinu na Ufundi, Dk.. Pascal Waniha, alieleza kuwa TMA imekuwa kielelezo bora katika ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na nje ya Kanda.

“Kazi kubwa imeendelea kufanyika katika kuiwakilisha nchi vizuri kwenye masuala ya hali ya hewa kimataifa na kueleza kuwa imeteuliwa na WMO kuwa muandaaji wa mafunzo ya rada katika Kanda ya Afrika yanayoratibiwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

“Fursa hii imepatikana kutokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya hali ya hewa unaoendelea kufanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Dk. Waniha.

Mafanikio mengine yaliyoelezwa mbele ya Katibu Mkuu kupitia mabango ni pamoja na maendeleo katika shughuli za uangazi, ununuzi wa vifaa na mitambo ya hali ya hewa, udhibiti wa huduma za hali ya hewa pamoja na njia mbalimbali zinazotumika katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa jamii na kwa sekta mahsusi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!