MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kimbunga ‘JOBO’ kipo umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia. Kimbunga hicho kimepungua nguvu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, tarehe 24 Aprili 2021 na TMA imesema, kimbunga hicho kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani.
“Hivyo, Jobo kwa sasa ni kimbunga hafifu kinachosafiri kwa kasi ya kilomita 18 kwa saa baharini,” imesema TMA
Hata hivyo, mamlaka hiyo ya hewa, imewashauri wananchi, kuendelea kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa za hali ya hewa.
Leave a comment