May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TMA: Kasi kimbunga JOBO imefifia

Spread the love

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imeeleza kwamba, kasi ya kimbunga JOBO imeendelea kufifia katika muda wa saa sita zilizopita. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Na kwamba, kuanzia sasa tishio la kimbunga hicho halipo Tanzania na kwamba, hakuna madhara ya moja kwa moja yanayotarajiwa.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili 2021 kwamba, kimbunga hicho kimefifia zaidi kilipotua kwenye Pwani ya Tanzania na Dar es Salaam.

TMA wameeleza, sababu kubwa ya kimbunga hicho kufifia ni kutokana na upepo kinzani na kwamba, mawingu makubwa yaliyoambatana na JOBO yamesambaa.

“Hali hii ilisababishwa na kuendelea kuimarika kwa upepo kinzani katika mwelekeo wa kimbunga cha Jobo,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza “mawingu ya mvua yaliyokuwa yameambatana na kimbunga hicho yamesambaa baharini karibuni na maeneo ya Kusini mwa Pwani ya Tanzania na Msumbiji.”.

Hata hivyo, taarifa hiyo imebainisha kuwa masalia ya mawingu yanayoambatana na kilichokuwa kimbunga yanaweza kusababisha mvua kwenye baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani.

error: Content is protected !!